DRC

DRC WAKIMBIZI MASHARIKI MWA CONGO WAOMBA KURUDI KWAO KULIKO KUWAPA MISAADA KILA SIKU KAMBINI.

MACHI 15, 2024
Border
news image

Varigenga DAVID ana miaka Zaidi ya arbaini ni mkimbizi kutoka mji wa Kichanga wilayani Masisi kwa sasa amechoshwa na hali ya ukimbizi katika kambi ya Bulengo magharibi mwa Mji wa Goma Kivu Kaskazini asema wakimbizi katika kambi mbali pembezoni mwa mji wa Goma Kivu kaskazini waomba serikali kuwarudisha nyumbani kwao kwa haraka kwani wamechoka sasa na hali ya ukimbizi na kushuhudia Maisha magumu kambini baada ya kukimbia makaazi yao ambako walikuwa kulima.

Msimamo unao kuwa nao Mugavo Heritier mkimbizi kutoka Masisi ipatikana kwa sasa katika Kambi ya wakimbizi ya Bulengo ambako ameshuhudia kifo cha Jirani wake kufariki Dunia baada ya kuangukiwa na Muti wakati wa Mvua ulio kuwa na kimbuka kikali Heritier anasema hali ya Maisha kwa sasa ni ngumu na wanao fanya vita lazima kuwanea huruma watu wanao taabika na Maisha hasa huduma za muhimu .

Hii ni baada ya watu wa wili kufariki Dunia na wenginzaidi ya ishirini kujeruhiwa wakati wa Mvua Kali ilio shuhudiwa katika kambi ya wakimbizi ya Bulengo pembeni ya ziwa Kivu .Mama Furahini Katalinda Hangi asema Jirani wake alifariki na kuacha Watoto kutokana na watu binafsi wanao sababisha maelefu ya watu kuhama makaazi yao na kuwa wakimbizi katika taifa lao.

Gavana wa Kiwa Kaskazini mwa Muda Meja Generali PETER CIRIMWAMI ameandamana hadi kambini na kamati ya usalama kuungana na falimia hathirika na kuwapa msaada wa Dola elfu kumi kujaribu kujibu mahitaji ya haraka kwa waathirika wa Mvua wengi ambao walipa chakula kikiharibiwa na Mvua na kwa sasa wakiwa hawana tena choo .

AM /MTV DRC ONLINE